'Mwenyezi Mungu' pekee ndiye anayeweza kunishawishi kuacha azma ya kuchaguliwa tena - Biden - BBC News Swahili (2024)

'Mwenyezi Mungu' pekee ndiye anayeweza kunishawishi kuacha azma ya kuchaguliwa tena - Biden - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ni "Bwana Mwenyezi Mungu" pekee ndiye anayeweza ku*mshawishi kusitisha azma yake ya kuchaguliwa tena, alipokuwa ameketi kwa ajili ya mahojiano ya nadra katika juhudi za kutuliza wasiwasi wa chama chake cha Democrats kuhusu azma yake ya kugombea.

Akiongea na ABC News mnamo Ijumaa, Bw Biden pia alikataa kufanya mtihani wa utambuzi na kuweka matokeo hadharani ili kuwahakikishia wapiga kura kwamba yuko sawa kuhudumu kwa muhula mwingine.

"Nina kipimo cha utambuzi kila siku. Kila siku nina mtihani huo - kila kitu ninachofanya [ni mtihani]," alimwambia mwandishi wa habari George Stephanopoulos.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 81 kwa mara nyingine alipuuzilia mbali wazo hilo, lililotolewa na baadhi ya maafisa wa Democrats na wafadhili, ambao walisema kwamba anapaswa kukaa kando ili apatikane mgombea kijana kufuatia kufanya vibaya katika mjadala wake na Donald Trump wiki iliyopita.

Wakati wote wa mahojiano, Bw Stephanopoulos alimshinikiza rais juu ya uwezo wake wa kuhudumu kwa muhula mwingine, akimuuliza Bw Biden ikiwa anakataa kukubali uhalisia kuhusu afya yake na uwezo wake wa kushinda.

"Sidhani kama kuna mtu yeyote aliye na sifa za kuwa rais au kushinda kinyang'anyiro hiki kuliko mimi," Bw Biden alisema, akilaumu utendaji wake duni wiki iliyopita kutokana na uchovu na "baridi mbaya." Katika mahojiano hayo ya dakika 22, pia:

  • Jaribio la kupunguza hofu ya Kidemokrasia ambapo alipoteza mwelekeo kwa Donald Trump tangu mjadala huo, akisema wapiga kura aliozungumza nao walisema kuwa kinyang'anyiro hicho ni "pigo"
  • Mapendekezo yaliyokataliwa washirika wanaweza kumwomba asimame kando. "Haitatokea," alisema
  • Alitupilia mbali maswali ya mara kwa mara kuhusu kile ambacho kingemlazimisha kuondoka kwenye kinyang'anyiro hicho. "Kama Mwenyezi Mungu angeshuka na kusema, 'Joe, ondoka kwenye kinyang'nyiro,' ningetoka kwenye kinyang'anyiro," alisema. "Mungu Mwenyezi hatashuka."

Rais alijibu maswali kwa ufasaha zaidi kuliko alivyofanya kwenye jukwaa la mjadala wiki iliyopita, lakini sauti yake tena ilionekana dhaifu na mara kwa mara.

Ilikuwa tofauti sana na utendaji wake katika mkutano wa hadhara huko Madison, Wisconsin, siku ya Ijumaa, ambapo Bw Biden mwenye nguvu alikubali utendaji wake mbaya katika mjadala wa CNN wa wiki iliyopita. "Tangu wakati huo, kumekuwa na uvumi mwingi. Joe atafanya nini?" aliuambia umati.

“Hili hapa jibu langu. Ninagombea na nitashinda tena,” Bw Biden alisema, huku wafuasi katika jimbo hilo muhimu la uwanja wa vita wakishangilia jina lake.

Unaweza pia kusoma:
  • Nani anayeweza kuchukua nafasi ya Biden ndani ya chama cha Democratic?

  • Uchaguzi wa Marekani 2024: Kubabaika kwa Biden katika mdahalo kwaongeza hofu kuhusu umri wake

'Mwenyezi Mungu' pekee ndiye anayeweza kunishawishi kuacha azma ya kuchaguliwa tena - Biden - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mahojiano na mkutano wa hadhara vinakuja wakati muhimu kwa kampeni yake, huku wafadhili na washirika wa Kidemokrasia wakitafakari iwapo watamuunga mkono au la.

Kampeni yake inafahamu kuwa siku chache zijazo zinaweza kuijenga au kuvunja azma yake ya kuchaguliwa tena, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za vyombo vya habari vya Marekani, huku Bw Biden akitafuta kurejesha imani iliyovunjwa na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump kufuatia mjadala huo.

Alipopanda jukwaani kwenye mkutano huo, Bw Biden alimpita mpiga kura mmoja ambaye alikuwa ameshika bango lililosomeka "Pitisha mwenge, Joe". Mpiga kura mwingine aliyesimama nje ya ukumbi alishika bango lililosomeka “Hifadhi urithi wako, acha!

"Ninaona hadithi hizi zote zinazosema mimi ni mzee sana," Bw Biden alisema katika mkutano huo, kabla ya kushinda rekodi yake katika Ikulu ya White House. "Je, nilikuwa mzee sana kuunda nafasi za kazi milioni 15?" alisema. "Je, nilikuwa mzee sana kufuta deni la wanafunzi kwa Wamarekani milioni tano?"

"Unadhani mimi ni mzee sana ku*mshinda Donald Trump?" aliuliza, huku umati ukijibu "hapana".

Akirejelea hukumu ya uhalifu ya Trump mjini New York, na mashtaka mengine anayokabiliwa nayo katika kesi tofauti, alimwita mpinzani wake "wimbi la uhalifu ".

'Mwenyezi Mungu' pekee ndiye anayeweza kunishawishi kuacha azma ya kuchaguliwa tena - Biden - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, Reuters

Baadhi ya wapiga kura katika mkutano wa hadhara wa Wisconsin wameimbia BBC kuwa wako tayari kubadilika.

Shinikizo kwa Bw Biden kujiuzulu limeongezeka tu kufuatia mjadala huo ambao ulikuwa na matukio kadhaa ambapo alipoteza mawazo yake mengi, na kuzua wasiwasi kuhusu umri wake na usawa wa akili.

Baadhi ya wafadhili wakuu wa chama cha Democratic wameanza ku*mshinikiza Bw Biden ajiuzulu kama mteule wa chama hicho, na kuonya hadharani kwamba watazuia pesa asipobadilishwa.

Kampeni yake inapanga kurudi kwa fujo. Mkewe, Jill Biden, pamoja na Makamu wa Rais Kamala Harris, wanapanga kampeni ya kuzunguka katika kila jimbo linapotarajiwa kuwa na mchuano mkali mwezi huu.

Bw Biden, ambaye anatarajiwa kuzungumza katika mkutano mwingine wa hadhara huko Pennsylvania siku ya Jumapili, alimshukuru makamu wa rais kwa msaada wake. Ameibuka kama mgombeaji anayewezekana zaidi kuchukua nafasi yake kwa tikiti ya Democratic ikiwa atajiuzulu.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa timu ya waandamizi wa Bw Biden inafahamu shinikizo linalotoka ndani ya Chama cha Democratic kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa kugombea wake ndani ya wiki ijayo.

Siku ya Ijumaa, ripoti ziliibuka kwamba kiongozi wa walio wachache katika Baraza la Wawakilishi Hakeem Jeffries alikuwa amepanga mkutano wa Jumapili na Wademokrat wakuu wa Baraza la Wawakilishi kujadili kugombea kwa Bw Biden.

Wanademokrasia wanne katika Baraza la Wawakilishi katika Bunge la Congress sasa wamemtaka ajiondoe kwenye kinyang'anyiro hicho - Lloyd Doggett wa Texas, Raúl Grijalva wa Arizona, Seth Boulton wa Massachusetts na Mike Quigley wa Illinois.

"Rais Biden amefanya utumishi mkubwa kwa nchi yetu, lakini sasa ni wakati wa yeye kufuata nyayo za baba yetu mwanzilishi, George Washington na kujitenga ili kuwaacha viongozi wapya wasimame dhidi ya Donald Trump," Bw Moulton aliambia kituo cha redio cha WBUR siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, hakuna Wademokrat waandamizi waliomtaka ajiuzulu, kama kampeni yake ilivyowadokezea waandishi wa habari.

Siku ya Ijumaa, ripoti ziliibuka kwamba Seneta Mark Warner alikuwa akijaribu kuunda kundi la maseneta wenzake wa chama cha Democratic kumwomba Bw Biden ajiondoe kwenye kinyang'anyiro hicho. Ripoti hizo, ikiwa ni pamoja na gazeti la Washington Post , zilisema kuwa Bw Warner alikuwa na wasiwasi mkubwa kufuatia mjadala wa CNN.

Akizungumza na wanahabari baadaye Ijumaa, Bw Biden alisema anaelewa kuwa Bw Warner "ndiye pekee anayezingatia hilo" na kwamba hakuna mtu mwingine aliyemtaka ajiuzulu.

Siku hiyo hiyo, Gavana wa Massachusetts Maura Healey, mwanademokrasia na mshirika wa Bw Biden, alitoa taarifa akimtaka rais "kutathmini kwa makini" ikiwa atasalia kuwa mgombea wa chama cha Democratic.

"Chochote ambacho Rais Biden ataamua, nimejitolea kufanya kila niwezalo ku*mshinda Donald Trump," alisema.

Unaweza pia kusoma:
  • Je, ni wakati wa viongozi wakongwe wa Marekani kustaafu?

  • Biden aapa ku*mshinda Trump baada ya kuyumba mwenye mdahalo

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi

'Mwenyezi Mungu' pekee ndiye anayeweza kunishawishi kuacha azma ya kuchaguliwa tena - Biden - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Lilliana Bartoletti

Last Updated:

Views: 5674

Rating: 4.2 / 5 (73 voted)

Reviews: 88% of readers found this page helpful

Author information

Name: Lilliana Bartoletti

Birthday: 1999-11-18

Address: 58866 Tricia Spurs, North Melvinberg, HI 91346-3774

Phone: +50616620367928

Job: Real-Estate Liaison

Hobby: Graffiti, Astronomy, Handball, Magic, Origami, Fashion, Foreign language learning

Introduction: My name is Lilliana Bartoletti, I am a adventurous, pleasant, shiny, beautiful, handsome, zealous, tasty person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.